FLORIDA, Marekani
MTOTO wa kiume wa nyota wa kikapu, LeBron James, Bronny, anajiandaa kurejea uwanjani baada ya kubainika tatizo lake la moyo aliozaliwa nalo.
Awali LeBron James alisema anataka kuendelea kucheza kwa muda mrefu zaidi ili aweze kucheza na mtoto wake huyo katika NBA.
James, ataendelea kucheza baada ya tatizo hilo la mtoto wake kujulikana.
Bronny, 18, alikuwa akisumbuliwa na shambulio la moyo wakati akiwa mazoezinio Chuo Kikuu cha Kusini cha California mwezi uliopita.
Hata hivyo alitolewa hospitalini Los Angeles baada ya siku tatu kupita.