Usyk atakiwa kuzichapa na Fury

LONDON, England

BONDIA wa uzito wa juu, Oleksandr Usyk, anapaswa kuzichana na Tyson Fury katika pambano la kuwania mikanda minne, amesema promota wa bondia Usyk.

Usyk, 36, atatetea ubingwa wa mikanda yake ya WBA (Super), WBO na IBF Jumamosi dhidi ya Muingereza Daniel Dubois.

Mazungumzo juu ya pambano hilo la kihistoria yanaendelea mbele ya muingereza huyo bingwa wa mkanda wa WBC ambapo awali mazungumzo yao yalivunjika mapema mwaka huu.

“Ni wajibu wetu kufanyika kwa pambano hili,” amesema Promota wa Usyk, Alexander Krassyuk.

“Mashabiki wote duniani wanataka kuona pambano hili. Na si sisi wenyewe au wanaohusika na ngumi, lakini watu wote ulimwenguni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *