Rais Samia apiga kura Uchaguzi mdogo Chamwino

1003626442-1-1024x724 Rais Samia apiga kura Uchaguzi mdogo Chamwino

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Novemba 04, 2026 amepiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Ofisi ya Kijiji cha Chamwino, mkoani Dodoma, katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino.

Uchaguzi huo unafanyika kwa lengo la kumpata Mbunge mpya wa Jimbo la Chamwino kufuatia aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Deogratius Ndejembi, kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1003626445-1024x796 Rais Samia apiga kura Uchaguzi mdogo Chamwino

Jumla ya wapiga kura 213,024 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wamepata fursa ya kushiriki kwenye Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma na Udiwani katika Kata 11 za Tanzania Bara leo.

Wapiga kura 133,864 wapo kwenye Jimbo la Chamwino na wapiga kura 79,160 wapo kwenye kata 11 zitakazofanya uchaguzi mdogo na kwamba, jumla ya vituo 665 vya kupigia kura vitatumika, ambapo vituo 441 vipo kwenye Jimbo la Chamwino na vituo 224 vipo kwenye kata 11 zitakazofanya uchaguzi mdogo.

1003626441-1024x728 Rais Samia apiga kura Uchaguzi mdogo Chamwino

Kata 11 zinazofanya uchaguzi huo kuwa ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza na Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.

1003626447-1024x736 Rais Samia apiga kura Uchaguzi mdogo Chamwino

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *