MANCHESTER, England
KIUNGO wa Manchester United, Mason Mount, atakosekana katika mechi mbili zijazo za Ligi Kuu ya England (EPL) kutokana na kuwa majeruhi.
Klabu hiyo imesema inatarajia kiungo huyo atarejea tena uwanjani baada ya kumalizika kwa mechi za kimataifa kutokana na kusumbuliwa na kuwashwa mwili wakati wa mechi yao dhidi ya Tottenham waliyofungwa 2-0.
Mount amejiunga na United akitokea Chelsea Juni kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni 55.
Kocha wa kikosi hicho, Erik ten Hag, kitaumana na Nottingham Forest Jumamosi kabla ya kusafiri kwenda kuumana na Arsenal Septemba 3.
Nyota huyo wa kimataifa wa England, Mount, 24, pia amezua hofu kucheza mechi za kufuzu Euro 2024 dhidi ya Ukraine itakayopigwa Septemba 9.