CINCINNATI, Marekani
MCHEZAJI nyota katika tenisi, Novak Djokovic, ameanza vizuri michuano ya Cincinnati Open kwa mara ya kwanza kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja nchini hapa ikipita miaka miwili.
Mshindi huyo mara 23 wa Grand Slam, hakuweza kushindana mashindano yoyote ndani ya nchi hiyo kutokana na kanuni za ugonjwa wa Uviko-19.
Lakini kanuni kwa wageni ambao hawakuchanja zilifanyiwa maboresho Mei na kumuwezesha nyota huyo kurejea katika mashindano.
Alishinda katika seti ya kwanza kwa 6-4 dhidi ya Mhispania Alejandro Davidovich Fokina, ambaye baadaye alishindwa kuendelea na mchezo kutokana na matatizo ya mgongo.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa nyota huyo, 36, wa kimataifa wa Serbia kwa mchezaji mmoja mmoja katika Cincinnati tangu 2019, ingawaje alipoteza Jumanne kwa wachezaji wawili wawili wakati akiwa na mwenzake, Nikola Cacic kutokana na kuchapwa na Muingereza, Jamie Murray na Michael Venus wa New Zealand.
“Nyakati zinakimbia. Miaka minne ni kama vile jana. Najisikia vizuri kurejea,” alisema nyota huyo namba mbili kwa ubora wa viwango duniani am