Venus Williams ang’ara Cincinnati Open

OHIO, Marekani

MCHEZAJI mkongwe katika tenisi, Mmarekani, Venus Williams, amemtandika Mrusi, Veronika Kudermetova ikiwa ni mara ya kwanza kwake kupata ushindi kwa mchezaji aliye chini ya nafasi ya 20 kwa ubora duniani ndani ya miaka minne katika michuano ya Cincinnati Open.

Williams, 43, amepambana kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa seti 6-4 7-5 dhidi ya Kudermetova ambaye ni wa 16.

Mshindi huyo mara saba wa mataji makubwa, alionesha kufurahia sana kwakuwa ni mara yake ya kwanza kushinda ikipita zaidi ya miaka mitatu.

“Naupenda huu mchezo, na ndivyo nilivyofanya,” amesema Williams, ambaye kwa ubora ni wa 533.

“Miaka kadhaa iliyopita imekuwa migumu kwaku kutokana na kuwa majeruhi lakini ninapenda niwepo hapa nikicheza, kuwa imara kama ninavyopaswa.”

Williams sasa ataumana na mshindi kati ya Mchina, Qinwen Zheng au Mbelarus, Aliaksandra Sasnovich katika raundi ya pili.

Nyota huyo namba moja wa zamani, ataangalia kushinda mfululizo kwa michuano hiyo ya WTA Tour kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019 mjini hapa.

Michuano hiyo pia ndio ya mwisho kwake kushinda dhidi ya mchezaji aliye ndani ya 20 Bora, akimfunga Kiki Bertens aliyekuwa namba tano wakati akiingia robo fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *