Tanzania Rasmi Kunufaika na Sh. Bilioni 461 za EU

IMG-20261017-WA0000 Tanzania Rasmi Kunufaika na Sh. Bilioni 461 za EU

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

UMOJA wa Ulaya (EU) umeidhinisha kuendelea kwa upatikanaji wa Euro milioni 156, sawa na takribani Shilingi bilioni 461, kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini Tanzania, baada ya kuchelewesha uidhinishaji wa fedha hizo kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Marc Stalmans, uamuzi huo ulifikiwa Julai 23, 2026, na unaruhusu utoaji wa fedha hizo kwa ukamilifu bila kupunguza bajeti wala kubadili malengo ya shughuli zilizopangwa awali.

Uamuzi huo unaashiria kuendelea kwa ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, ambao ni miongoni mwa washirika muhimu wa nchi katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

EU inaunga mkono maendeleo ya sekta za kilimo, nishati, miundombinu, biashara na teknolojia, ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Ulaya, biashara kati ya Tanzania na EU ilifikia Euro bilioni 2.15 mwaka 2025, hali inayoonesha ukubwa wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *