Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji

WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.08.27-1024x683 Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji

Na Mwandishi Wetu, Dodoma, Oktoba 13, 2026

SERIKALI imewasilisha Bungeni mkakati wa kuboresha uchimbaji, udhibiti, uongezaji thamani na biashara ya Tanzanite, kwa lengo la kuongeza tija kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa ndani na kuinua ushindani wa madini hayo katika soko la kimataifa.

Akiwasilisha mkakati huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema soko la Tanzanite linakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwamo wafanyabiashara wasiofuata taratibu, kupungua kwa uzalishaji, utoroshaji wa madini na ushindani kutoka kwa vito mbadala vinavyotengenezwa viwandani.

Amesema Serikali inalenga kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzanite (Tanzanite Exchange Centre) na kuweka mfumo rasmi wa minada.

Hatua hizo zinatarajiwa kuongeza uwazi katika biashara na kuhakikisha Tanzanite inaongezewa thamani nchini kabla ya kusafirishwa.

“Lengo letu ni kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wa vito wazawa kuuza madini yao kwa bei shindani inayoendana na soko la dunia. Tutafikia hilo kupitia mifumo thabiti ya uthaminishaji wa madini,” amesema Mavunde.

Waziri huyo pia amesema Serikali itafanya utafiti wa kina katika eneo la Mirerani na maeneo yaliyo nje ya ukuta wa mgodi ili kubaini maeneo mapya yenye viashiria vya Tanzanite.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Subira Mgalu, ameitaka Serikali kuongeza juhudi za kuitangaza Tanzanite katika masoko makubwa ya kimataifa.

Amesema Tanzania, ambayo ndiyo nchi pekee duniani inayozalisha madini hayo, inapaswa kutambulika katika mnyororo mzima wa thamani wa Tanzanite ili kunufaika zaidi kiuchumi.

Mgalu pia ameipongeza Wizara ya Madini kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27.

Katika mwaka huo wa fedha, Wizara ya Madini inalenga kukusanya Sh. trilioni 1.406. Mwenendo wa ukusanyaji katika robo ya kwanza unaashiria uwezekano wa kufikia au kuvuka lengo hilo.

WhatsApp-Image-2026-10-13-at-06.51.13-1-1024x683 Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-06.51.13-1024x683 Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-06.51.12-1-1024x683 Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-06.51.12-1024x683 Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-06.51.11-1-1024x683 Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-06.51.11-1024x683 Serikali Kuimarisha Biashara ya Tanzanite na Kudhibiti Utoroshaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *