Dira 2050 inahitaji mabadiliko ya fikra -Kafulila

IMG-20260704-WA0009-1024x681 Dira 2050 inahitaji mabadiliko ya fikra -Kafulila

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-Centre), David Kafulila, amesema ili Tanzania ifikie uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050 kunahitajika ongezeko la uzalishaji na mabadiliko ya kasi ya maendeleo.

Amesema lengo hilo linahitaji kiwango cha uzalishaji kinacholingana na kile kilichopatikana katika kipindi cha miaka 25 iliyopita (2000 hadi 2025).

Kafulila ametoa kauli hiyo kwenye mhadhara wa umma uliofanyika Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Mbeya Ijumaa Julai 03, 2026 alisema changamoto iliyopo ni kuhakikisha taifa linaelewa ukubwa wa dhamira hiyo.

Amesema lengo la Dira ya Maendeleo 2050 linahitaji mtazamo mpya wa pamoja katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, vijiji na taifa kwa ujumla ili kuhakikisha uzalishaji na tija vinaongezeka kwa kiwango kikubwa zaidi.

Tanzania inalenga kuingia kundi la nchi 21 duniani zenye uchumi wa dola trilioni moja, Rais Samia Suluhu Hassan alipozindua Dira ya Maendeleo 2050 alisisitiza lengo hilo linawezekana endapo kutakuwa na mabadiliko ya msingi ya namna ya kufikiri na kutenda kwa wananchi na taasisi mbalimbali,”alisema

Kafulila ameongeza kuwa iwapo taifa litaendelea na mtazamo uleule wa zamani katika ngazi ya mtu binafsi, kijiji na taifa, lengo hilo linaweza lisifikiwe au kufikiwa kwa kiwango cha chini, akisisitiza mafanikio yatategemea “total turnaround” ya fikra na utekelezaji katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii ili kufanikisha mabadiliko ya kweli kuelekea mwaka 2050.

IMG-20260704-WA0003-1024x767 Dira 2050 inahitaji mabadiliko ya fikra -Kafulila
IMG-20260704-WA0008-1024x681 Dira 2050 inahitaji mabadiliko ya fikra -Kafulila

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *