Arsenal yaacha watatu ziara Marekani

LONDON, England

KLABU ya Arsenal, imeenda nchini Marekani kwa ajili ya kuendelea na kambi kujiandaa na msimu mpya huku ikiacha nyota wake watatu.

Mchezaji mpya, kiungo Declan Rice, ameambatana na wachezaji wenzake katika safari hiyo.

Nyota walioachwa katika kikosi hicho kitakachoenda kujipima nguvu kesho na MLS All-Stars ni Nicolas Pepe, Albert Sambi Lokonga na Cedric Soares huku pia Emile Smith-Rowe na Thomas Partey wataungana na wenzao wiki ijayo.

Wachezaji hao wengine inaelezwa wapo katika mchakato wa kuachwa na klabu hiyo.

Kikosi cha Mikel Arteta, ikimaliza mchezo huo, itaumana pia na Manchester United na Barcelona kabla ya kurejea Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *