TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi

WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.39.16-1-1024x575 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi

Na. Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI yatembelea ofisi za Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Makao Makuu Dodoma. Juni 10, 2026 kwa lengo la kujionea utendaji wa taasisi inavyotekeleza majukumu yake.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Johannes Lukumayi, amesema lengo la kamati ni kujionea kwa macho namna taasisi hii muhimu katika kulinda afya ya jamii imejipanga katika kuwahakikishia wananchi wanalindwa afya yao kupitia bidhaa za dawa na vifaa tiba.

“Tunafahamu umuhimu wa taasisi hii ndani ya nchi katika kulinda afya zetu na nje ya nchi pia katika kuongoza taasisi nyingine,” amesema Lukumay.

Akichangia wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Adonis Bitegeko, aliipongeza Mamlaka kwa mapinduzi makubwa katika kuwekeza katika mifumo ya TEHAMA na aliitaka Mamlaka kuendelea kutatua changamoto ya mifumo ya uingizaji mizigo kwa kushirikiana na wadau wengine kufuatia mabadiliko yaliyopo katika mfumo huo.

Aidha alitoa wito kwa Mamlaka kujipanga ili kuendana na ukuaji wa sayansi na Tecknolojia katika masuala ya udhibiti.

Ziara hiyo pia ilihusisha viongozi wa Wizara ya Afya akiwamo Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalage ambao kila mmoja aliipongeza Mamlaka kwa utendaji na namna inatekeleza majukumu yake.

WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.38.24-1024x575 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi
WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.38.23-1024x575 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi
WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.39.16-2-1024x575 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi
WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.39.17-1-1024x575 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi
WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.39.17-1024x575 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi
WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.39.18-2-1024x682 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi
WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.39.18-1-1024x682 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi
WhatsApp-Image-2026-06-12-at-02.39.18-1024x575 TMDA yaikosha Kamati ya Bunge, Masuala ya Ukimwi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *