Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi

WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.24-2-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,

RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Comrade Tumaini Nyamhokya, ametoa wito kwa wanahabari nchini kuwa daraja kati ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na wafanyakazi pamoja na wategemezi wao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu fidia kwa wafanyakazi kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanaofanya Kazi katika Vyombo vya Habari (JOWUTA), leo Mei 25, 2026 jijini Dar es Salaam, Nyamhokya amesema waandishi wa habari wana nafasi ya kipekee ya kufikisha elimu kwa umma kuhusu kazi na huduma zinazotolewa na taasisi mbalimbali, hususan WCF.

Ameeleza kuwa mafunzo haya yamekusudia kuongeza uelewa wa wanahabari kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi, ili waweze kuripoti kwa usahihi na kuhamasisha waajiri kujisajili katika WCF na kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

Aidha, amewataka wanahabari kuelimisha waajiri juu ya umuhimu wa kuripoti kwa wakati matukio ya ajali, ugonjwa au vifo vinavyotokana na kazi, hatua itakayosaidia WCF kuchakata na kutoa fidia stahiki kwa walengwa.

Nyamhokya amesisitiza kuwa WCF ni taasisi ya wafanyakazi, iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263, na inalenga kushughulikia fidia kwa wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi wanaopata madhila kutokana na kazi zao.

Amebainisha kuwa mfuko huo unatoa mafao mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu, fidia ya ulemavu wa muda au wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, msaada wa mazishi na malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki kutokana na kazi.

Aidha, ameipongeza JOWUTA kwa kuratibu mafunzo haya na kuwaleta pamoja wanachama wake, akisema kuwa kujengea uwezo wanachama ni nyenzo muhimu kwa uhai wa chama chochote cha wafanyakazi. Aliongeza kuwa kupitia taaluma yao, wanahabari wana jukumu la kuhamasisha wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuunganisha nguvu katika kutetea maslahi yao.

Akihitimisha hotuba yake, Nyamhokya amewakumbusha washiriki kauli mbiu ya wafanyakazi duniani “Solidarity Forever”, akisisitiza mshikamano na umoja kama msingi wa mafanikio katika mapambano ya kudai haki za wafanyakazi.

WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.29-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.28-2-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.28-1-1024x810 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.27-1-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.27-1-1-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.27-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.26-1-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.26-1024x600 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.25-1-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.25-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.25-1-1-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.24-1-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-07.21.25-2-1024x683 Waandishi wa Habari watakiwa kuwa daraja kati ya WCF na wafanyakazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *