JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF

WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.48.15-1-1024x722 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Mussa Juma Siwayombe, ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini, kuhakikisha wanahabari wanasajiliwa katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wanachama wa JOWUTA kuhusu fidia kwa wafanyakazi leo Mei 25,2025 jijini Dar es Salaam, Siwayombe amesema ni wajibu wa waajiri kuzingatia sheria za kazi kwa kuwapa wanahabari ajira za kudumu au mikataba rasmi.

Amesisitiza kuwa bila usajili na ajira za kudumu, wanahabari wanakosa haki ya kupata stahiki zao, ikiwamo huduma za matibabu, fidia ya ulemavu, msaada wa mazishi na malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki kutokana na kazi.

Mafunzo hayo, yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na WCF, yamekusanya wanachama wa JOWUTA kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Siwayombe ameeleza kuwa mafunzo haya ni mwanzo wa safari ya kupeleka elimu hiyo katika kanda nyingine za nchi, ikiwamo Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.

Aidha, ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kazi kwa jitihada zake za kutatua changamoto zinazowakabili wanahabari.

Amebainisha kuwa wataanza ziara maalum hivi karibuni kubaini waajiri wanaotumia wanahabari bila mikataba ya ajira, hatua ambayo inalenga kulinda haki za wafanyakazi wa sekta ya habari.

Siwayombe amesisitiza mshikamano wa JOWUTA na Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA), ameeleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha wanahabari wanapata haki sawa na sekta nyingine.

Ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wanahabari nchini hawana ajira za kudumu, jambo linalohitaji hatua za haraka za kisheria na kiutendaji.

Akihitimisha hotuba yake, Siwayombe aliwakumbusha wanahabari kauli mbiu ya wafanyakazi duniani “Solidarity Forever”, akisisitiza mshikamano na umoja kama msingi wa mafanikio katika kudai haki za wafanyakazi.

Mafunzo haya yanafungua ukurasa mpya wa matumaini kwa wanahabari nchini, huku JOWUTA ikiahidi kuendelea kushirikiana na WCF na TUCTA kuhakikisha tasnia ya habari inakuwa na mazingira bora ya kazi na heshima kwa wafanyakazi.

WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.48.05-1024x708 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.48.15-1024x722 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.48.26-1024x673 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.48.35-1024x682 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.48.42-1024x682 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.49.17-1024x682 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-04.49.23-1-1024x682 JOWUTA yawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwasajili wanahabari WCF

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *