TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026

WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.57-1024x682 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kuanza kwa msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti mwaka 2026.

Mwezi Juni unatarajiwa kuwa na hali ya baridi katika maeneo mengi ya nchi, huku mwezi Julai ukitajwa kuwa na vipindi vya baridi kali zaidi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 25,2026 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria, Kanda ya Magharibi, Kusini pamoja na Nyanda za Juu Kusini-Magharibi yanatarajiwa kuwa na hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi.

Dkt. Chan’ga amesema maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini na Kusini pamoja na Mkoa wa Dodoma yanatarajiwa kuwa na hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani.

Kwa upande wa baadhi ya maeneo yenye miinuko yakitarajiwa kushuka hadi chini ya nyuzi joto 10 za sentigredi.

“Msimu huu utatawaliwa na upepo kutoka Kusini Mashariki wenye nguvu iliyopungua kidogo, lakini kutakuwapo vipindi vya upepo mkali zaidi katika miezi ya Juni na Julai hususan kwenye maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi na baadhi ya maeneo ya nchi kavu,” amesisitiza Dkt. Chang’a.

Aidha, TMA imeeleza kuwa licha ya msimu wa Kipupwe kwa kawaida kuwa wa ukavu, baadhi ya maeneo yanatarajiwa kupata mvua za nje ya msimu, ikiwamo Kanda ya Ziwa Victoria hususan Mkoa wa Mara pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.

Hata hivyo TMA imetahadharisha kuwa hali ya baridi na vumbi inaweza kuongeza magonjwa yanayohusiana na mfumo wa upumuaji kama mafua na homa ya mapafu, pamoja na magonjwa ya macho na yale yanayoathiri mifugo.

“Mamlaka inazitaka jamii, wakulima, wafugaji pamoja na wadau wa sekta mbalimbali kuchukua tahadhari na kuendelea kufuatilia utabiri wa hali ya hewa pamoja na tahadhari zinazotolewa ili kuongeza usalama na ufanisi wa shughuli zao za kila siku,” amesisitiza Dkt. Chan’ga.

TMA itaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa mrejesho hivyo watumiaji wa taarifa za utabiri wanashauriwa kufuatilia na kuzingatia utabiri wa saa 24, siku 19, mwezi pamoja na tahadahari za hali mbaya ya hewa.

WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.55-1024x927 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.52-1024x682 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.50-1024x682 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.40-1024x682 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.43-1024x682 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.39-1024x682 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026
WhatsApp-Image-2026-05-25-at-01.39.34-1024x682 TMA yatangaza Msimu wa Kipupwe kuanzia Juni hadi Agosti, 2026

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *