Bei ya Dezeli na Petroli Kenya yapaa zaidi ya Tanzania

bei-1024x576 Bei ya Dezeli na Petroli Kenya yapaa zaidi ya Tanzania

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya (EPRA) imetangaza ongezeko jipya la bei ya mafuta, hatua iliyosababisha Kenya kuwa na bei kubwa zaidi za mafuta ukilinganisha na Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Mei 2026, bei ya petroli nchini Kenya imepanda kwa Sh za Kenya 16.65 hadi kufikia KSh. 214.25 kwa lita, sawa na takribani Shilingi za Tanzania 4,300. Dizeli nayo imeongezeka kwa KSh. 46.29 hadi KSh. 242.92 kwa lita, sawa na karibu TSh. 4,860.

Kwa upande wa Tanzania, bei za mafuta zilizotangazwa na EWURA mwezi Mei 2026 zinaonyesha kuwa petroli inauzwa kwa wastani wa TSh. 4,115 kwa lita huku dizeli ikiwa TSh. 4,248 katika jiji la Dar es Salaam.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Petroli ya Kenya ni ghali kwa takribani TSh.185 zaidi kwa lita ukilinganisha na Tanzania na Dizeli ya Kenya ni ghali kwa zaidi ya TSh. 600 kwa lita kuliko Tanzania.

Wachambuzi wa uchumi wanaeleza kuwa tofauti hiyo inachangiwa na ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia, kodi za mafuta nchini Kenya pamoja na gharama za usafirishaji.

Ongezeko hilo linatarajiwa kuongeza gharama za usafiri, bidhaa na huduma nchini Kenya, huku Tanzania ikiendelea kuwa na nafuu kidogo katika sekta ya mafuta ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

WhatsApp-Image-2026-05-14-at-10.36.21-1024x1024 Bei ya Dezeli na Petroli Kenya yapaa zaidi ya Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *