Salome azindua Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA – PRIS

WhatsApp-Image-2026-05-14-at-11.32.43-1024x682 Salome azindua Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA - PRIS

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema uzinduzi wa Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA – PRIS ni hatua muhimu katika kuimarisha uchumi wa kisasa unaotegemea teknolojia ndani ya sekta ya mafuta.

Amesema sekta ya nishati ni mhimili wa uchumi wa Taifa, hivyo matumizi ya mifumo ya kidijitali yataongeza ufanisi wa huduma pamoja na kukuza matumizi ya teknolojia nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa PRIS (Puma Retail Information System), jana jijini Dar es Salaam, Salome amesema mfumo huo ni teknolojia ya kisasa ya itakayosaidia kusimamia shughuli za vituo vya mafuta ikiwamo mauzo, malipo, usimamizi wa stoki za mafuta pamoja na taarifa za biashara kwa wakati halisi.

Ameeleza kuwa mfumo huo unalenga kuongeza ufanisi, uwazi na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja, sambamba na kuboresha usimamizi wa biashara za mafuta nchini.

Aidha, Salome ameipongeza Puma Energy Tanzania kwa kuendelea kuwekeza nchini kupitia ubunifu wa kidijitali, upanuzi wa vituo vya mafuta na uwekezaji katika nishati safi ya CNG.

Amesema mfumo huo unaendana na malengo ya Tanzania ya kujenga uchumi wa kidijitali kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Mkakati wa DESF 2024–2034.

Mfumo wa PRIS tayari umeonyesha mafanikio katika nchi za Malawi na Zimbabwe kabla ya kuanza kutumika Tanzania, huku Serikali ikieleza kuwa ubunifu huo utasaidia kuongeza ubora wa huduma na kukuza ujumuishi wa kiuchumi kwa wananchi.

WhatsApp-Image-2026-05-14-at-11.32.38-1024x682 Salome azindua Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA - PRIS
WhatsApp-Image-2026-05-14-at-11.32.38-1-1024x682 Salome azindua Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA - PRIS
WhatsApp-Image-2026-05-14-at-11.32.39-1024x682 Salome azindua Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA - PRIS
WhatsApp-Image-2026-05-14-at-11.32.40-1024x678 Salome azindua Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA - PRIS
WhatsApp-Image-2026-05-14-at-11.32.40-1-1024x664 Salome azindua Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA - PRIS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *