Waziri wa Mambo ya nje Belarus afanya ziara nchini

WhatsApp-Image-2026-04-27-at-21.14.39-1024x683 Waziri wa Mambo ya nje Belarus afanya ziara nchini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Belarus, Maxim Ryzhenkov, ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia leo Aprili 28 hadi 30, 2026, kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Ryzhenkov aliwasili nchini jana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo alipokewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Belarus nchini Mhe.Dzmitry Krasouski.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Ryzhenkov anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, leo Aprili 28, 2026, jijini Dar es Salaam. Aidha, atakutana na viongozi wengine wa Serikali kwa lengo la kuendeleza na kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus pamoja na kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

WhatsApp-Image-2026-04-27-at-21.14.38-1024x683 Waziri wa Mambo ya nje Belarus afanya ziara nchini
WhatsApp-Image-2026-04-27-at-21.14.37-1-1024x683 Waziri wa Mambo ya nje Belarus afanya ziara nchini
WhatsApp-Image-2026-04-27-at-21.14.37-1024x683 Waziri wa Mambo ya nje Belarus afanya ziara nchini
WhatsApp-Image-2026-04-27-at-21.14.34-1024x683 Waziri wa Mambo ya nje Belarus afanya ziara nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *