WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, ameliomba Bunge kuidhinisha jumla ya bajeti ya Sh. trilioni 2.5 kwa ajili ya Wizara ya Nishati na taasisi zake kwa mwaka 2026/27 ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu yaliyopangwa.
Amefafanua kuwa kati ya fedha hizo, asilimia 97.5 sawa na zaidi ya Sh. trilioni 2.46 zitatumika kwenye miradi ya maendeleo, huku fedha za ndani zikichangia sehemu kubwa na zilizobaki zikiwa ni fedha za nje.
Ndejembi aliongeza kuwa, asilimia 2.5 ya bajeti hiyo, sawa na zaidi ya Sh. bilioni 63, zitatumika kwa matumizi ya kawaida ikiwamo gharama za uendeshaji na mishahara ya watumishi wa wizara pamoja na taasisi zake kama PURA.



