Waziri Mkuu atimiza ahadi ya kitimwendo kwa Helena Joseph

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Aprili 20, 2026) amemkabidhi kitimwendo Helena Joseph Mwandu (mwenye mahitaji maalum), Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. 

Waziri Mkuu aliahidi kumpatia Helena kiti hicho katika mazungumzo waliyoyafanya baada ya mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Msanga wilayani Chamwino Dodoma, jana (Aprili 19, 2026).

Akizungumza baada ya kupatiwa kiti hicho, Helena amemshukuru Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu kwa kumpatia kitimwendo hicho kwani kitamsaidia katika shughuli zake.

WhatsApp-Image-2026-04-20-at-07.10.45-1024x576 Waziri Mkuu atimiza ahadi ya kitimwendo kwa Helena Joseph
WhatsApp-Image-2026-04-20-at-07.08.40-1-1024x576 Waziri Mkuu atimiza ahadi ya kitimwendo kwa Helena Joseph
WhatsApp-Image-2026-04-20-at-07.08.39-1-1024x576 Waziri Mkuu atimiza ahadi ya kitimwendo kwa Helena Joseph

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *