Ndejembi ashiriki maonesho kongamano la nishati safi ya kupikia Morogoro

WhatsApp-Image-2026-03-17-at-01.15.16-1024x869 Ndejembi ashiriki maonesho kongamano la nishati safi ya kupikia Morogoro

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, ameshiriki maonesho ya Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia yanayofanyika leo mkoani Morogoro.

Kongamano hilo limehusisha wizara na taasisi mbalimbali za umma kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali zikiwamo taasisi za fedha pamoja na wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nishati safi ya kupikia.

Kongamano limeandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na taasisi ya uongozi likiwa na kaulimbiu ya ‘Kuimarisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Maendeleo Endelelevu’.

Kutoka Wizara ya Nishati, Ndejembi ameongozana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Nolasco Mlay.

WhatsApp-Image-2026-03-17-at-01.15.14-1024x683 Ndejembi ashiriki maonesho kongamano la nishati safi ya kupikia Morogoro
WhatsApp-Image-2026-03-17-at-01.15.12-1024x683 Ndejembi ashiriki maonesho kongamano la nishati safi ya kupikia Morogoro
WhatsApp-Image-2026-03-17-at-01.15.10-1024x683 Ndejembi ashiriki maonesho kongamano la nishati safi ya kupikia Morogoro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *