Prof. Kabudi, Balozi Nyalandu kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Madola

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Kazi Maalum Ikulu, Palamagamba Kabudi, akiambatana na Lazaro Nyalandu, Balozi na Mshauri wa Rais katika masuala ya Diplomasia, wataiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Commonwealth of Nations unaofanyika nchini Uingereza.

Katika mkutano huo wa kimataifa, ujumbe huo wa Tanzania pia utawasilisha ujumbe maalum wa Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan, unaobeba msimamo na dira ya nchi katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kukuza diplomasia ya uchumi, pamoja na kuendeleza mazungumzo ya kimkakati yanayolenga ustawi wa pamoja wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Ushiriki huo unaakisi dhamira ya Tanzania kuendelea kuwa mshiriki hai katika majukwaa ya kimataifa, huku ikiimarisha nafasi yake ya kidiplomasia na kuendeleza ushirikiano unaochochea maendeleo, biashara na utulivu katika jumuiya ya kimataifa.

WhatsApp-Image-2026-03-07-at-02.50.45 Prof. Kabudi, Balozi Nyalandu kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Madola

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *