Rais Samia ateua majaji 6 mahakama ya rufani

UTEUZI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewateua Majaji sita wa Mahakama ya Rufaa

Amemteua Jaji Zainab Goronya Muruke kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Kabla ya uteuzi huo, Jaji Muruke alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi – Temeke, Dar es Salaam

Jaji Dkt. Benhajj Shaaban Masoud ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masoud alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria Tanzania

Naye Jaji Amour Said Khamis ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Khamis alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora

Aidha Rais Samia amemteua Jaji Leila Edith Mgonya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgonya alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu Dar es Salaam

Amemteua Jaji Gerson John Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mdemu alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma

Pia amemteua Jaji Agnes Zephania Mgeyekwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgeyekwa alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Uteuzi huo wa Majaji wa Mahakama ya Rufani umeanza tarehe 28 Aprili, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *