HALMASHAURI SIMAMIENI USAFI WA BARABARA -MATIVILA

1001019899-1024x768 HALMASHAURI SIMAMIENI USAFI WA BARABARA -MATIVILA

Na Mwandishi Wetu, Iringa

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi-Tamisemi anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu zoezi la usafi wa barabara, akisisitiza kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu.

Mhandisi Mativila amesema hayo leo Mei 13, 2025, mkoani Iringa wakati wa ukaguzi wa Ujenzi wa Barabara ya Wenda–Mgama Km.19 inayojengwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE kwa gharama ya Sh. bilioni 29.7 ambayo imefikia asilimia 99 ya utekelezaji.

Mhandisi Mativila alisema usimamizi mzuri wa barabara unahitajika ili kuhakikisha barabara hizo zinadumu na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.

1001019904-1024x768 HALMASHAURI SIMAMIENI USAFI WA BARABARA -MATIVILA

“Ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa barabara hizi zinatunzwa, hasa kwa kuhakikisha zinaendelea kuwa safi na salama kwa matumizi. Hili ni jukumu la pamoja,” amesema Mativila.

Ameongeza kuwa uwepo wa barabara bora unachochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kuwawezesha wananchi kusafirisha bidhaa na huduma kwa urahisi, hali inayosaidia kuongeza mapato ya halmashauri kupitia ushuru na tozo mbalimbali.

1001019906-1024x768 HALMASHAURI SIMAMIENI USAFI WA BARABARA -MATIVILA

Aidha, Mhandisi Mativila ametoa onyo kwa wakandarasi wazembe wanaoshindwa kutekeleza miradi kwa viwango vilivyokusudiwa au kuchelewesha kazi, akisema serikali haitasita kuwachukulia hatua kali.

“Serikali inataka kuona thamani ya fedha inaonekana katika kila mradi na hatutavumilia uzembe unaokwamisha juhudi hizi za maendeleo,” amesisitiza.

1001019907-1024x576 HALMASHAURI SIMAMIENI USAFI WA BARABARA -MATIVILA

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Wenda–Mgama ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha miundombinu ya vijijini kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi.

1001019905-1024x768 HALMASHAURI SIMAMIENI USAFI WA BARABARA -MATIVILA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *