Kikwete awasilisha ujembe wa Rais Samia kwa Serikali ya Niger

Na Mwandishi Wetu

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo na Rais wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani katika Ikulu ya Niamey April 16, 2025.

Katika mazungumzo hayo, Kikwete ambaye ni mwanadiplomasia nguli aliwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Jenerali Tchiani.

Aidha, katika mazungumzo hayo, Kikwete aliwasilisha salamu za Rais Samia ambapo alielezea kufurahishwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Niger na kusisitiza umuhimu wa kukuza na kuuimarisha zaidi katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii.

Alisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kubadilishana uzoefu na ujuzi ili utajili mkubwa wa maliasili uliopo uweze kuvunwa na kuendelezwa kwa faida ya wananchi wa bara hilo.

1000859301-1024x682 Kikwete awasilisha ujembe wa Rais Samia kwa Serikali ya Niger
1000859297-1024x678 Kikwete awasilisha ujembe wa Rais Samia kwa Serikali ya Niger
1000859299-1024x682 Kikwete awasilisha ujembe wa Rais Samia kwa Serikali ya Niger
1000859304-1024x675 Kikwete awasilisha ujembe wa Rais Samia kwa Serikali ya Niger

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *