Samia atoa bil. 56/- za miradi ya maji

Na Mwandishi Wetu, Manyara

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa Shs. bilioni 56 kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maji mijini na vijijini mkoani Manyara katika kipindi cha miaka mitatu.

Kati ya miradi hiyo, 64 tayari imekamilika na kuzalisha skimu 347.

Mkuu wa Mkoa huo, Queen Sendiga, aliyasema hayo wakati akishuhudia utiaji saini mikataba ya miradi ya maji kwenye vijiji ndani ya halmashauri sita yenye gharama ya Shs. 9,685,375,945.51.

Kupitia Miradi hiyo, wananchi 83,624 wanatarajiwa kunufaika kupitia vituo 140 vitakavyojengwa.

Sendiga amewataka Wakandarasi kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba kwa muda, ubora.

Meneja wa RUWASA mkoani humo, Mhandisi Walter Kirita, aliitaja miradi iliyosainiwa ni Gijedaboshka katika Wilaya ya Babati, Gunyoda-Mbulu, Endamaghay-Babati,  Madunga-Babati, Muguchi-Hanang, Naberera-Simanjiro.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Manyara, Peter Toima, alisema CCM kitaendelea kuisimamia ipeleke huduma za kijamii maeneo yote.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Wilaya mkoani humo, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Kheri James alisema lazima miradi hiyo iwafikie wananchi wote kama serikali ya awamu ya sita inavyosisitiza huduma ya maji kwa kila kijiji ili kimtua mama ndoo kichwani.

Mhandisi Jumanne Werema kwa niaba ya Wakandasi wengine, waliahidi kutekeleza miradi hiyo kwa mujibu wa mikataba.

Alisema amefanya kazi ya Uhandisi kwa miaka 27 lakini RUWASA mkoani Manyara ni sehemu pekee ambayo wana utaratibu mzuri unaowawezesha Wakandarasi kufanya kazi kwa ushirikiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *