Wakurugenzi, Ma-RC kueleza majukumu yao

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

IDARA ya Habari (Maelezo), imeandaa programu ya kuwakutanisha Wakuu wa Mikoa (RC), Wakurugenzi wa Halmashauri zote kwenye kila mkoa pamoja ili waeleze utekelezaji wa masuala mbalimbali katika maeneo yao.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, aliyasema hayo alipozungumza na Wahariri wa vyombo vya habari. “Mikutano hii ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi itaanza Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam,  Awamu ya pili itafanyika katika mikoa ya Manyara, Arusha, Tanga na Kilimanjaro,” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *