Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UWEKEZAJI katika Bandari ya Dar es Salaam utaiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuongeza mapato yanayotokana na bandari kutoka asilimia 40 hadi asilimia 67.
Uwekezaji huo ni fursa kubwa kwa maendeleo kwa Watanzania na sekta mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari.
“Uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia DP World utaiwezesha TRA kuongeza mapato yanayotokana na Bandari kutoka asilimia 40 hadi 67,” alieleza.
“Tanzania inapakana na nchi nane ambazo tukitumia fursa hii vizuri itachochea kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi,” alisema Matinyi.