Mvua kubwa kunyesha siku nne – TMA

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA), imetoa angalizo ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kwa siku nne kuanzia jana Oktoba 30, 2023.

Mvua hiyo itanyesha katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa mujibu wa Mamlaka hiyo, mvua hizo zimeanza kunyesha jana hadi Novemba 2, 2023 ikiwa na kiwango cha wastani cha athari zinazoweza kutokea.

Taarifa imeeleza kuwa, athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi ya watu kujaa maji, kuathirika baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *