Mradi wa bandari kavu EPZA kukamilika Januari, 2027

MRADI wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, kupitia ujenzi wa eneo la kuhifadhi makasha katika Bandari Kavu ya EPZA, Kurasini, umefikia asilimia 90 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika Januari 2027.

Hatua hiyo imelenga kupunguza msongamano bandarini na kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena.

1003724229 Mradi wa bandari kavu EPZA kukamilika Januari, 2027

Mradi huo utakapokamilika utawezesha kuhifadhi makasha 700,000 kwa mwaka, ambapo eneo la kwanza (Phase One) litakuwa na uwezo wa kuhifadhi makasha 150,000, huku eneo la pili likiwa na uwezo wa makasha 550,000.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo leo Novemba 12, 2026 Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema uwekezaji huo utawezesha baadhi ya taratibu za ukaguzi wa makasha, ikiwemo uchunguzi kwa kutumia mashine (scanning) na ukaguzi wa kimwili, kufanyika katika eneo hilo badala ya ndani ya bandari.

1003723980 Mradi wa bandari kavu EPZA kukamilika Januari, 2027

“Utaratibu huo utaanza kwa makasha ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi (export), kabla ya kuhusisha makasha ya bidhaa zinazoingia nchini (import), hatua itakayosaidia kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam,”amesema.

Mbarawa amesema mradi huo ni sehemu ya manufaa ya uwekezaji unaofanyika bandarini, akieleza kuwa mwekezaji anayetekeleza mradi huo pia amepewa dhamana ya kuendesha Kituo cha kuhudumia makasha namba mbili (Terminal 2).

Amezitaka TPA, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha barabara maalumu zitakazotumika kuhudumia eneo hilo zinafanyiwa kazi haraka ili kuwezesha mradi kuanza kutumika kwa wakati uliopangwa.

1003724195-1024x683 Mradi wa bandari kavu EPZA kukamilika Januari, 2027

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bandari, Abed Gallus Abed, alisema Bandari ya Dar es Salaam inatarajia kuhudumia zaidi ya makasha milioni 1.5 mwaka huu, ikilinganishwa na makasha milioni 1.3 yaliyohudumiwa mwaka jana.

Amesema ongezeko la shehena limekuwa likisababisha changamoto ya maeneo ya kuhifadhi makasha, hivyo kukamilika kwa Kurasini Logistic Park kutasaidia kupokea shehena inayoongezeka na kupunguza msongamano unaotokana na taratibu za ukaguzi ndani ya bandari.

1003717633-1024x1024 Mradi wa bandari kavu EPZA kukamilika Januari, 2027

“Eneo hili litakuwa na mashine za kutosha za ukaguzi wa makasha (scanners), zitakazosaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa shehena,”amesema.

Amemhakikishia Waziri kuwa kwa mujibu wa mpango uliowekwa, ifikapo Januari 2027 eneo hilo litaanza kufanya kazi, ambapo awali litaanza kuhudumia makasha kupitia ICD, kabla ya kuanza shughuli za upanuzi wa bandari (Port Extension) baada ya mashine za ukaguzi kuwasili.

1003717612-1024x1024 Mradi wa bandari kavu EPZA kukamilika Januari, 2027

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *