Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS

Ni Baada ya Mjadala wa Kina na Wanachama

IMG_4939-1024x574 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BAADA ya mvutano wa muda mrefu, hatimaye leo wanachama wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA) wamepata fursa ya kusomewa na kujadili mkataba kati ya TAFFA na Capital Pay International kuhusu utekelezaji wa Mfumo wa Tanzania Clearing Agents Minimum Agency Fee System (TCAMS).

Katika mkutano huo, wanachama walipata nafasi ya kutoa maoni, kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mfumo huo.

Miongoni mwa masuala muhimu yaliyopewa kipaumbele ni uhakikisho kwamba fedha za wanachama hazitakatwa kupitia mfumo huo, gharama za mfumo hazitatokana na Agency Fees, na kwamba makato ya asilimia 30 yaliyokuwa yakitajwa awali siyo utaratibu uliowasilishwa kwa wanachama.

Baada ya majadiliano na kupokea ufafanuzi, wanachama wengi waliridhia mfumo huo. Zaidi ya wanachama 300 walipiga kura ya kuunga mkono mfumo, huku wanachama watano pekee wakipiga kura ya kutouridhia. Matokeo hayo yanaonesha uamuzi wa wengi kuunga mkono hatua za kuendeleza mfumo huo.

Rais wa TAFFA alisisitiza dhamira ya uongozi ya kulinda maslahi ya wanachama, kuhakikisha uwazi katika utekelezaji wa mfumo, na kuzingatia matakwa ya kisheria yaliyowekwa na Serikali kupitia GN Na. 83 ya mwaka 2026, hususan matakwa yanayohusu matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kuripoti na kutangaza ada za huduma za clearing and forwarding.

Aliongeza kuwa utekelezaji wa mfumo huo unalenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na uzingatiaji wa viwango vya chini vya ada za huduma, huku ukisaidia sekta ya clearing and forwarding kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na kutokuzingatia matakwa ya kisheria.

Kupitishwa kwa TCAMS kunafungua hatua mpya kwa TAFFA katika kuendeleza mifumo ya kidijitali inayolenga kulinda maslahi ya wanachama, kuimarisha utendaji wa sekta na kuhakikisha utekelezaji wa GN Na. 83 unafanyika kwa uwazi na kwa kuzingatia sheria.

IMG_4951-1024x980 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS
IMG_4939-1-1024x574 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS
IMG_4938-1024x978 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS
IMG_4940-1-1024x683 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS
IMG_4947-1024x553 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS
IMG_4925-1024x567 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS
IMG_4926-1024x943 Wanachama wa TAFFA Wapatiwa Mfumo wa TCAMS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *