
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
FAINALI ya mashindano ya kutafuta Miss Ilala 2026, ilifanyika Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutika ukumbi wa The Dreamer’s Lounge ambapo Celine Mollel ametwaa taji hilo mwaka huu.
Mashindano hayo ya Miss Ilala yalishirikisha warembo 13, ambapo nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Celine Mollel, mshindi wa pili Hadija Azary ,mshindi wa tatu Irene Yoram,mshindi wa nne Karen Angelo na nafasi ya tano bora imechukuliwa na Rosemary Galibona .
Akizungumza katika Fainali hiyo ya Miss Ilala, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Nurudini Bilal, ametumia fursa hiyo kuwapongeza waandaaji wa mashindano hayo ambayo yalikuwa na ushindani mkubwa kwa warembo kushindana.
Meya Nurudini Bilal amesema kwa niaba ya Halmashauri mwakani Halmashauri ya jiji itaweka nguvu kubwa sababu ya kuitangaza Wilaya ya Ilala ndani na nje kwani warembo wa miss Ilala wamepata tiketi ya kushiriki Miss Dar es Salaam kutokana na uzuri wa Warembo wa Ilala watapata tiketi ya kushiriki Miss Tanzania na Taji la Miss Tanzania mrembo atatoka Ilala.
Aidha, amesema warembo hao wa Ilala walioingia tano bora katika masuala ya urembo umiss utawapa ajira mbalimbali na kupata fursa za kiuchumi.
Diwani wa Kata ya Chanika Gaudence Kashoka amesema, Ilala ndio jiji linaloongoza kwa mapato Tanzania kupitia mashindano hayo warembo hao wataenda kuitangaza Ilala na vivutio vyake vya kitalii.
Mkurugenzi wa mashindano hayo Lucas Rutainurwa, ametoa zawadi zenye thamani ya Sh. milioni 7.4 ambapo mshindi namba moja alijinyakulia Sh. milioni 2, mshindi wa pili milioni 1,500,000 mshindi wa tatu milioni 1,000,000, mshindi wa nne Sh. 800,000 na mshindi wa tano Sh.500,000.
Rutainurwa pia ametoa kifuta jasho Sh. 200,000 kila mmoja kwa washiriki wanane ambao warishiriki mashindano hayo lakini hawakufanikiwa kushinda.
Mratibu mkuu wa mashindano ya kumtafuta Miss Ilala Yasinta Mtayabarwa,amesema warembo wake waliopata tiketi ya kushiriki miss Dar es Salaam kwa sasa wanaenda kujiandaa wakisubiri kwenda kambini na Ilala wamejipanga kuchukua mataji yote.



