Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino

WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.13.03-1024x682 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino

Na Mwandishi Wetu, Babati

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Nkoba Mabula ameielekeza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Tarangire kwakushirikiana na Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuendelea na tathmini na maboresho ya miundombinu ya mawasiliano pamoja na kutoa mafunzo kwa maafisa na askari waliopo katika vikosi vya uokoajii kulingana na maandalizi ya kukabiliana na mvua za El Niño na athari zake.

Akizungumza katika ziara hiyo leo Oktoba 20, 2026 alipotembelea Hifadhi ya Taifa Tarangire, Mabula alieleza kuwa mikakati ya kukabiliana na mvua hizo imelenga kulinda shughuli za uhifadhi na utalii zisisimame wala kuathiriwa kwa kiwango kikubwa pindi mvua hizo zitakapoanza.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Kurugenzi ya Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara Izumbe Msindai alieleza kuwa kila hifadhi imefanya jitihada za mapema kukabiliana na mvua hizi na inaombwa Wizara kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Shirika ili kulinda mapato na kuboresha mazingira rafiki kwa wageni wa nje na ndani ya nchi.

Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Tarangire Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George alieleza kuwa mbali na matengenezo ya mitambo 6 ya utengenezaji wa barabara na uokoaji, Hifadhi imefanikiwa kuanzisha timu ya haraka ya kukabiliana na dharura kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Babati kutoka katika azimio la kikao kilichofanyika mnamo Oktoba 6, 2026.

Aidha Kamishna Dkt. Tutindaga aliongeza kuwa Hifadhi kwa kushirikiana na wadau utalii hususani watoa huduma za malazi imeimarisha mifereji ya maji katika barabara za kitalii kwa kufanya light grading na kufukia mashimo sambamba na kuchimba mitaro ili kuzuia maji kutuama kwenye barabara.

Katika Ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu alipata wasaa wa kukagua miundombinu iliyofanyiwa maboresho, mitambo ya matengenezo ya barabara na uokoaji, uwanja wa ndege wa kuro, malango ya kupokelea wageni, shughuli za ukataji wa vibali na njia za mawasialiano ya dharura.

WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.13.05-1024x682 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino
WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.13.06-1024x682 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino
WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.13.07-1024x712 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino
WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.13.09-1024x682 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino
WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.13.10-1024x682 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino
WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.13.11-1024x819 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino
WhatsApp-Image-2026-10-20-at-07.12.55-1024x683 Tarangire Yajipanga Kukabiliana na Mvua za El-Nino

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *