Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi

WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.58.14-1024x770 Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi

Na Mwandishi Wetu, Katavi

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameagiza kuharakishwa kwa miradi ya barabara, maji na umeme mkoani Katavi, huku akiwataka wakandarasi wanaosuasua kuongeza kasi ya utekelezaji ili wananchi waanze kunufaika na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali.

Maagizo hayo ametoa alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, akiwa njiani kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, ambapo alipata fursa ya kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumpokea.

Akizungumzia changamoto ya umeme, Makamu wa Rais ameitaka TANESCO kuhakikisha kufikia Desemba 01 2026, Mpanda inapelekewa Transfoma itakayoongeza megawati 50 zaidi za umeme ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka katika Manispaa ya Mpanda na maeneo mengine ya mkoa huo.

Makamu wa Rais amesisitiza kuhakikisha ahadi ya kukamilisha maboresho hayo inatekelezwa, sambamba na kuweka nguzo za zege.

WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.58.13-1024x683 Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.58.11-1024x768 Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.58.09-1024x683 Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.58.08-819x1024 Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.58.07-819x1024 Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi
WhatsApp-Image-2026-10-13-at-07.58.05-819x1024 Makamu wa Rais Awabana Wakandarasi wa Barabara, Maji na Umeme Katavi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *