Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania ikishirikiana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vichwa vya treni nchini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uwezo wa viwanda vya ndani na kupanua uzalishaji wa bidhaa nchini.
Dkt. Samia amesema uwekezaji huo ni sehemu ya azma pana ya nchi kuongeza uzalishaji viwandani, kutengeneza fursa za ajira na kupunguza utegemezi wa bidhaa za viwandani zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.
Ametoa kauli hiyo Novemba 19, 2026 nchini Uganda, alipokuwa akihutubia hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuunganisha magari cha Double Q Motors, huku akisisitiza umuhimu wa maendeleo ya viwanda katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki.
“Ningependa kutumia fursa hii kuwajulisha kuwa kwa sasa Tanzania kushirikiana na wadau ajili ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vichwa vya treni. Hii ni sehemu ya azma yetu pana ya kuimarisha uzalishaji wa ndani na uwezo wa viwanda,” amesema Rais Samia.



