Rais Samia: Zahanati, vituo vya afya vyafikia 13,683

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeongeza zahanati na vituo vya afya nchini hadi 13,683, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji unaolenga kusogeza huduma karibu na wananchi na kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi, mama na mtoto.

Hatua hiyo imeenda sambamba na ongezeko la hospitali za wilaya kutoka 117 hadi 174, hospitali za rufaa za mikoa kutoka 21 hadi 28 na hospitali za taifa na maalumu kufikia 13, huku zaidi ya asilimia 85 ya Watanzania wakipata huduma za afya ndani ya kilomita tano kutoka maeneo wanayoishi.

1003898796-1024x683 Rais Samia: Zahanati, vituo vya afya vyafikia 13,683

Akizungumza leo Novemba 26,2026 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe (RMNCAH+N), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji huo umechangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka 556 hadi 76, hatua inayoonesha umuhimu wa kuboresha huduma za afya, uongozi na uwajibikaji.

1003898800-1024x683 Rais Samia: Zahanati, vituo vya afya vyafikia 13,683

Amesema mafanikio hayo yameifanya Tanzania kuwa na uzoefu muhimu wa kushirikisha mataifa mengine ya Afrika katika mapambano dhidi ya vifo vinavyoweza kuzuilika, akibainisha kuwa vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 24 hadi 17 kwa kila vizazi hai 1,000, huku vya watoto walio chini ya miaka mitano vikishuka kutoka 43 hadi 28.

“Tumekwenda kufanya kazi, waganga wetu, madaktari wetu, wauguzi wetu wamekwenda kuchapa kazi na kupunguza vifo hivi hadi 76,” alisema Rais Samia, ambaye mwaka huu amepewa dhamana ya kuwa Kinara wa Umoja wa Afrika (AU) wa Afya ya Mama na Mtoto.

1003898791-1024x683 Rais Samia: Zahanati, vituo vya afya vyafikia 13,683

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *