Rais Samia: Tanzania imepiga hatua kupunguza vifo vya uzazi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya vifo vitokanavyo na uzazi, baada ya kuvipunguza kutoka 556 hadi 76.

Amesema hatua hiyo inaonesha matokeo ya uwekezaji wa Serikali katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.

1003898802-1024x675 Rais Samia: Tanzania imepiga hatua kupunguza vifo vya uzazi


Mafanikio hayo yanaiweka nchi katika nafasi muhimu ya kushirikisha mataifa mengine ya Afrika uzoefu wa kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika, wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akitekeleza dhamana ya kuwa Kinara wa Umoja wa Afrika (AU) wa Afya ya Mama na Mtoto.


Akizungumza leo Novemba 26,2026 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe (RMNCAH+N), Rais Samia amesema mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja za Serikali na watumishi wa sekta ya afya katika kuboresha huduma na kuokoa maisha.

1003898788-1024x683 Rais Samia: Tanzania imepiga hatua kupunguza vifo vya uzazi


Amesema mwaka 2023 wakati Tanzania ilipotunukiwa tuzo ya Goalkeepers Award na Gates Foundation, vifo vya uzazi vilikuwa vimepungua kutoka 556 hadi 104, kabla ya kushuka zaidi hadi 76 katika takwimu za mwaka 2024/2025.


“Zawadi ile ilitupa nguvu zaidi. Tumekwenda kufanya kazi, waganga wetu, madaktari wetu, wauguzi wetu wamekwenda kuchapa kazi na kupunguza vifo hivi hadi 76,” amesema.

1003898778-1024x721 Rais Samia: Tanzania imepiga hatua kupunguza vifo vya uzazi


Mafanikio mengine yaliyotajwa ni kupungua kwa vifo vya watoto wachanga kutoka 24 hadi 17 kwa kila vizazi hai 1,000 na vya watoto walio chini ya miaka mitano kutoka 43 hadi 28.

Rais Samia amesema Serikali inalenga ifikapo mwaka 2030 kupunguza vifo vya uzazi hadi 70 kwa kila vizazi hai 100,000, vifo vya watoto wachanga hadi 12 na vya watoto chini ya miaka mitano hadi 25 kwa kila vizazi hai 1,000.

1003898801-1024x683 Rais Samia: Tanzania imepiga hatua kupunguza vifo vya uzazi
1003898755-1024x683 Rais Samia: Tanzania imepiga hatua kupunguza vifo vya uzazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *