Prof. Shemdoe Ataka Kila Wanafunzi wa Darasa la Wawe Mahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kupitia Umoja wao wa Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA), kuhakikisha kila mwanafunzi anapofika darasa la tatu anakuwa na umahiri wa kutosha katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), hatua itakayoweka msingi imara wa mafanikio ya elimu.

Prof. Shemdoe ameeleza kuwa, Walimu Wakuu wakifanikiwa kuhakikisha wanafunzi wanaofika darasa la tatu wanamudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), ufaulu katika upimaji wa darasa la pili na la nne utaongezeka kwa ubora unaostahili.

Prof. Shemdoe amesema hayo jana Novemba 24, 2026 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa TAPSHA, unaohudhuriwa na Wenyeviti wa Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara, uliofanyika katika Ukumbi wa New Generation Hall jijini Dodoma.

“Walimu Wakuu lengo lenu liwe ni kuwezesha stadi za KKK, kwani tukifanikiwa kila mtoto wa darasa la tatu kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana,” amesisitiza Prof. Shemdoe.

Ameongeza kuwa, mafanikio hayo yataakisi kaulimbiu ya mkutano huo isemayo “Mafanikio ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kila mtoto ni msingi imara wa maarifa na ujuzi kwa maendeleo ya taifa, wajibu wetu, mafanikio yetu”, hivyo ni jambo jema kwa Walimu Wakuu kutambua kuwa wana wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wanapofika darasa la tatu wanamudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, jambo litakalochangia mafanikio katika stadi hizo za KKK.

Aidha, Prof. Shemdoe amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuongeza bajeti ya ruzuku ya uendeshaji katika sekta ya elimu, hatua ambayo imewezesha kuendelea kulipa posho za madaraka kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari na Maafisa Elimu nchini, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kukarabati na kujenga miundombinu mipya kwa lengo la kuimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Naye, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Bw. Atupele Mwambene, amesema matarajio ya mkutano huo ni kuimarika kwa stadi za KKK na matokeo ya elimu kwa mwaka ujao, kutokana na Walimu Wakuu kupata fursa ya kujitathmini na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza ufaulu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti TAPSHA, Mwalimu Rehema Ramole, ameishukuru Serikali kupitia OWM–TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na wadau wa elimu kwa kutekeleza mikakati mbalimbali katika kuimarisha kikamilifu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

WhatsApp-Image-2026-11-24-at-21.02.58-1024x682 Prof. Shemdoe Ataka Kila Wanafunzi wa Darasa la Wawe Mahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)
WhatsApp-Image-2026-11-24-at-21.02.34-1024x683 Prof. Shemdoe Ataka Kila Wanafunzi wa Darasa la Wawe Mahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)
WhatsApp-Image-2026-11-24-at-21.02.31-1024x683 Prof. Shemdoe Ataka Kila Wanafunzi wa Darasa la Wawe Mahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)
WhatsApp-Image-2026-11-24-at-21.02.32-1024x683 Prof. Shemdoe Ataka Kila Wanafunzi wa Darasa la Wawe Mahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)
WhatsApp-Image-2026-11-24-at-21.10.46-1024x683 Prof. Shemdoe Ataka Kila Wanafunzi wa Darasa la Wawe Mahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *