
Rais Samia Suluhu Hassan na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, amesema Tanzania imepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyotokana na uzazi, akieleza kuwa idadi hiyo imeshuka kutoka 556 mwaka 2019 hadi 104 mwaka 2023.
Amesema mafanikio hayo yaliifanya Tanzania kutambuliwa na kupewa tuzo na Gates Foundation mwaka 2022 na 2023, jambo lililoongeza hamasa ya Serikali kuimarisha zaidi huduma za afya ya mama na mtoto.
Rais Samia ameyasema hayo leo Novemba 23, 2026 katika Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Ameeleza kuwa utafiti wa hivi karibuni ambao anatarajia kuuzindua Novemba 26, 2026, unaonyesha kuwa vifo vya wajawazito vimeendelea kushuka hadi takribani 75 kwa kila vizazi hai 100,000, huku vifo vya watoto vikishuka kutoka 63 hadi 43.


