REA yawajengea uwezo viongozi wake kwa itifaki na maadili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWANADIPLOMASIA mwandamizi, Balozi Omar Kashera Mjenga, ndc, amewajengea uwezo wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhusu itifaki na maadili ya kiuongozi.Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha weledi, uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya viongozi.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amewataka viongozi kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na taratibu za kiitifaki.

1003818286-1024x560 REA yawajengea uwezo viongozi wake kwa itifaki na maadili

Amesema misingi hiyo ni muhimu katika mawasiliano rasmi, mahusiano ya kikazi na ushirikiano na wadau wa maendeleo.

Mhandisi Saidy ameongeza kuwa uzingatiaji wa itifaki huimarisha nidhamu na kujenga taswira nzuri ya REA.

Kwa upande wake, Balozi Mjenga ameeleza misingi ya itifaki, mawasiliano rasmi na mwenendo unaofaa kwa viongozi.

1003818283-1024x685 REA yawajengea uwezo viongozi wake kwa itifaki na maadili

Amesisitiza umuhimu wa kulinda heshima na hadhi ya Taasisi katika utekelezaji wa majukumu ya kiuongozi.

Aidha, Afisa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Franco Haule, ametoa mafunzo kwa Menejimenti ya REA kuhusu usimamizi wa vikao kupitia mfumo wa eBoard.

Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha viongozi kutumia mfumo huo katika kuandaa, kusimamia na kufuatilia vikao kwa ufanisi, pamoja na kurahisisha upatikanaji na usimamizi wa nyaraka za vikao kwa njia ya kidijitali.

1003818287-1024x536 REA yawajengea uwezo viongozi wake kwa itifaki na maadili

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za REA za kuimarisha uwezo wa Menejimenti, kuongeza ufanisi katika usimamizi wa vikao na kuboresha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi.

Jitihada hizo pia zinalenga kuongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi ya nishati vijijini na kuboresha huduma za nishati zinazotolewa kwa wananchi.

1003818288-1024x569 REA yawajengea uwezo viongozi wake kwa itifaki na maadili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *