Mafanikio ya Mpango wa Afya Afrika Yatapimwa kwa Maisha Yatakayookolewa

WhatsApp-Image-2026-11-23-at-04.32.27-1-1024x672 Mafanikio ya Mpango wa Afya Afrika Yatapimwa kwa Maisha Yatakayookolewa

Rais Samia Suluhu Hassan na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, amesema mafanikio ya Mpango wa Bara la Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana hayatapimwa kwa ahadi za viongozi pekee, bali kwa maisha yatakayookolewa kupitia utekelezaji wake.

Amesema mafanikio halisi yataonekana pale mama atakapovuka salama kipindi cha kujifungua, mtoto mchanga anapopata mwanzo mzuri wa maisha, kila mtoto anapolindwa kwa chanjo na kijana anapowezeshwa kutimiza uwezo wake.

Rais Samia amesema hayo leo, Novemba 23, 2026 katika Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Ametaka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuweka waratibu wenye mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo na kuingiza malengo yake matatu katika mikakati ya kitaifa ya afya.

#SamiaKinaraAfrika
#AfyaMamaNaMtoto

WhatsApp-Image-2026-11-23-at-04.32.28-1-1-1024x683 Mafanikio ya Mpango wa Afya Afrika Yatapimwa kwa Maisha Yatakayookolewa
WhatsApp-Image-2026-11-23-at-04.32.28-2-1024x633 Mafanikio ya Mpango wa Afya Afrika Yatapimwa kwa Maisha Yatakayookolewa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *