Rais Samia Atangaza Ufadhili Wataalam wa Afya 60 Afrika

WhatsApp-Image-2026-11-23-at-04.32.28-1024x683 Rais Samia Atangaza Ufadhili Wataalam wa Afya 60 Afrika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza ufadhili wa awali wa nafasi 60 za mafunzo ya kibobezi na ya juu katika taaluma mbalimbali za afya kwa nchi za Afrika, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na upungufu wa wataalamu wa afya katika bara hilo.

Nafasi hizo zitajumuisha mafunzo katika fani za ukunga, usingizi na ganzi, uzazi na magonjwa ya wanawake pamoja na huduma za watoto wachanga, kwa lengo la kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi maalumu na kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto.

Rais Samia amesema hayo leo Novemba 23,2026 wakati akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Amesema mafunzo hayo yatawahusisha pia wataalamu wa ngazi ya kati, wauguzi na wakunga, ili kuongeza uwezo wao katika kutoa huduma salama za uzazi, huduma za dharura, matumizi ya ganzi na huduma muhimu kwa watoto wachanga.

Rais Samia amebainisha kuwa upungufu wa wataalamu wa afya wenye utaalamu maalumu ni miongoni mwa changamoto zinazoathiri utoaji wa huduma bora za afya barani Afrika, hivyo mpango huo unatarajiwa kuchangia kuimarisha rasilimali watu na mifumo ya afya katika nchi za Afrika.

#SamiaKinaraAfrika
#AfyaMamaNaMtoto

WhatsApp-Image-2026-11-23-at-04.32.27-1024x682 Rais Samia Atangaza Ufadhili Wataalam wa Afya 60 Afrika
WhatsApp-Image-2026-11-23-at-04.32.28-1-1024x683 Rais Samia Atangaza Ufadhili Wataalam wa Afya 60 Afrika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *