Jukwaa la Uwekezaji zao la Mwani lazinduliwa Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefungua Jukwaa la Uwekezaji la Zao la Mwani Zanzibar 2026 leo tarehe 18 Novemba 2026 Mkoa wa Mjini Magharibi, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha usarifu wa mwani na uzalishaji wa bidhaa zenye thamani kubwa ili kuongeza kipato cha wakulima, ajira na kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Buluu.

1003801684-1024x682 Jukwaa la Uwekezaji zao la Mwani lazinduliwa Zanzibar

Amesema Serikali imeweka sekta ya Uchumi wa Buluu katika nafasi muhimu ya mageuzi ya uchumi wa Zanzibar, hivyo itaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa, kilimo cha mwani katika kina kirefu cha bahari, upatikanaji wa mbegu bora na tafiti za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya ukaushaji, uhifadhi, ukusanyaji na usarifu wa mwani ili kuongeza ubora wa zao hilo, kupunguza upotevu baada ya mavuno na kuwawezesha wakulima kunufaika zaidi na shughuli zao.

1003801685-1024x682 Jukwaa la Uwekezaji zao la Mwani lazinduliwa Zanzibar

Rais Dkt. Mwinyi amewakaribisha wawekezaji wenye mitaji, teknolojia na utaalamu kuwekeza katika sekta hiyo, akisisitiza umuhimu wa uwekezaji utakaowezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika, kuongeza ajira kwa vijana na kuwashirikisha wananchi katika mnyororo mzima wa thamani wa zao la mwani.

Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amezindua Zanzibar Seaweed Investment Promotion Deal Book, inayobainisha fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora, teknolojia za kilimo, ukaushaji, uhifadhi, usarifu wa viwandani na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na mwani kwa matumizi ya vyakula, vipodozi, dawa na kilimo.

1003801695-1024x672 Jukwaa la Uwekezaji zao la Mwani lazinduliwa Zanzibar

Viongozi mbalimbali wamehudhuria wakiwemo wa Serikali, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, wawekezaji, taasisi za fedha, washirika wa maendeleo, watafiti, sekta binafsi, wakulima na wadau mbalimbali wa zao la mwani kutoka ndani na nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *