TALGWU yawanoa watumishi wa umma na waajiri Dar


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimeendesha mafunzo maalum kwa watumishi wa umma na waajiri mkoani Dar es Salaam, yakilenga kuimarisha mahusiano bora kazini na kuhakikisha utekelezaji wa haki na wajibu wa kila upande kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Ofisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Mgonja, aliyemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa, amesema kuwa TALGWU imekuwa kiunganishi muhimu kati ya waajiri na wafanyakazi, kwa kuhakikisha maslahi ya watumishi yanalindwa bila kuathiri ustawi wa taasisi.
“Sehemu ya kazi ni mahali ambapo mtumishi anapaswa afurahie kuwepo. Uhusiano mwema huchangia amani, utulivu na usalama wa mahali pa kazi. TALGU wamefanya kazi kubwa kuhakikisha mijadala baina ya waajiri na wafanyakazi inaleta uelewano,” amesema Mgonja.
Aidha, TALGWU ilisisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali na waajiri katika kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi na ya Taifa yanalindwa kwa usawa. Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa chama huo kutoa elimu, kuimarisha utendaji, na kujenga mshikamano kazini.

“Maofisa utumishi na wakurugenzi jambo kubwa sana la umuhimu ni kuwafahamu watumishi wetu unaweza ukamuona mtu kila siku anachelewa kazini kumbe ana matatizo ambayo anapaswa kusikilizwa.


“Tunatakiwa kujua ni namna gani tunaweza kuweka mazingira
bora ya watu, wapo watumishi ambao wanaamka asubuhi hawatamani kwenda kazini kwa sababu ya maofisa rasilimali watu, wakurugenzi ipo sehemu anaitwa Mungu mtu hii inamfanya mtu achukie kazi,”amesema Mgonja.
Amesema ni muhimu kwa kila ofisi kuweka mazingira mazuri ya kazi ili mtumishi akiamka atamani kufanya kazi na kwenda kazini.
Awali Naibu Katibu Mkuu TALGWU, Wandiba Ngocho,
amesema chama chao ndiyo chama ambacho kinatetea wafanyakazi waliopo chini ya mamlaka ya serikali za mitaa ukiacha walimu kuna kundi kubwa la wanaowatetea.
“Kitu muhimu kinafanywa na chama ni kuwafanya wafanyakazi kuwa karibu sana na wanachama wake ni utaratibu wetu kama chama tunakutana na wadau hawa kila mwaka mwisho wa siku hii ni kama kioo tunajitathimini kila mwaka.
“Tumefanya hii kila mikoa lakini leo ni zamu ya Mkoa wa Dar es Salaam, tunawashukuru waajiri pamoja na changamoto nyingi lakini tuna uhusiano mzuri,”amesema Ngocho.
Amesema chama huwa kina utaratibu wa mazungumzo wanakaa wanaongea na waajiri pia kuna watendaji wa mitaa vijiji tunataka wafanye kazi kwakutumia kanuni na utaratibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *