Ununuzi helkopta za wagonjwa ‘wanukia’

Na Mwandishi Wetu, Dar e Salaam

SERIKALI ya Awamu ya Sita ipo katika mazungumzo ya kununua helikopta za kubebea wagonjwa (air ambulance) ambazo zitatoa huduma maeneo yasiyofikika kirahisi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania 2022, jijini Dar es Salaam.

Alisema Wizara hiyo inafanya mazungumzo na Wizara za Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na pamoja na Wizara ya Fedha ili kufanikisha mpango huo.

Ametolea mfano maeneo yasiyofikika kirahisi ni pamoja na Mafia, Loliondo, visiwa vya Ukerewe.

Mwalimu aliongeza kuwa, pia Serikali inatarajia kuanzisha mfumo wa taifa ya uratibu na matumizi ya magari ya kubeba wagonjwa (ambulance).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *