
Tanzania kwa kushirikiana na Nigeria itaandaa Mkutano wa Kwanza wa Afya ya Wanawake Afrika (Women’s Health Africa Summit), utakaofanyika Desemba 1, 2026, kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa ahadi za kisiasa na uwajibikaji katika kufikia malengo ya Sifuri Tatu (Three Zeros), yanayolenga kuhakikisha kila mjamzito anajifungulia katika kituo cha kutolea huduma za afya, kukomesha vifo vya kina mama na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika, pamoja na kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mkutano huo pia utalenga kuimarisha maendeleo ya watumishi wa sekta ya afya pamoja na utoaji wa huduma za afya katika ngazi ya jamii.
Rais Samia amesema hayo leo, Novemba 23, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026) na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika, uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia.
#SamiaKinaraAfrika
#AfyaMamaNaMtoto


