Na Sarah Moses, Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linafanyika kwa siku saba ambapo limeanza leo Machi 17,2925 na litamalizika Machi 23, 2025.
Hayo ameyasema leo Machi 17 ,2025 jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema zoezi hilo linawahusu watu waliotimiza umri wa miaka 18 au wanaokusudia kutimiza miaka hiyo.
Amesema kuwa, zoezi hilo halihusishi kubadilisha kadi zilizotolewa na iliyokuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015 na mwaka 2020 kadi hizo zote ni halali .
“Zoezi hili pia litahusisha kutoa kadi kwa watu ambao wamepoteza kadi zao au kuharibika,” amesema Chalamila.
Ameongeza kuwa zoezi Hilo litawawezesha wapiga kura walio hama maeneo mbalimbali kujitokeza kwaajili yakuweza kuhuisha taarifa zao upya.
Pamoja na hayo RC Chalamila amewaomba wananchi wa Mkoa huo wenye sifa kujitokeza katika zoezi hilo la siku saba nakusema kuwa taarifa zinazosambaa mtandaoni zakuhamasisha watu wasijitokeze kujiandikisha zipuuzwe kwasababu wanaofanya hivyo wameshajiandikisha.
“Ninayo shauku yakwamba kila mtu atajitokeza kufanya jambo hilo kama ilivyokusudiwa.” amesema.
mwisho.