Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amevunja ukimya dhidi ya wanasiasa wa upinzani wanaodai makali yake ya kisiasa yamekwisha.
Wanasiasa hao walikwenda mbali zaidi na kumuita Kabwe ‘CCM B’.
Akijibu madai hayo kupitia kipindi cha Medani za Siasa cha Star TV, Kabwe alisema haoni tabu kuitwa ‘CCM B’, hizo ni promaganda za kisiasa ambazo ni za kawaida.
Alisema wakati CHADEMA kikifanya vizuri katika ulingo wa siasa za Tanzania, vyama vya NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF) viliitwa CCM B.
“Acha watuite CCM B’ muhimu ni sisi ACT-Wazalendo kusimama katika reli kwa yale ambayo tunayasimamia, ufanyaji wa siasa hauwezi kufanana na wao.
“Sisi si chama cha ajenda moja, tunazungumzia masuala yote ya wananchi, chama chetu sio cha kupiga kelele na kubwabwaja-bwabwaja.
“Inatopotea changamoto ya kitaifa utatuona, hatuishii kusema tu bali tunapendekeza namna ya kufanya na kuna muda serikali inatekeleza tunachokipendekeza,” alisema.