Na Badrudin Yahaya
KLABU ya Yanga, imeanza vibaya kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa CR Belouizdad ya nchini Algeria.
Mabao ya Belouizdad katika mchezo huo yamefungwa na Raouf Benguit na
Abdulrahman Meziane ambao walifunga kabla ya mapumziko.
Kwenye kipindi cha pili dakika za lala salama, Yanga walijikuta wakiruhusu bao la tatu lililofungwa na Lamin Jallow ambaye alifunga muda mfupi baada ya kuingia.
Baada ya matokeo hayo, Yanga sasa wanarejea nyumbani katika uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapokea Al Ahly katika mchezo wa pili ambao utafanyika, Desemba 2.
Mchezo dhidi ya Belouizdad ni wa kwanza kwa Yanga kwenye hatua ya makundi baada ya miaka 25.