Wood kumvaa Warrington kutetea ubingwa wa Dunia

LONDON, England

BONDIA Leigh Wood, atatetea ubingwa wake wa Dunia mkanda wa WBA uzito wa unyoya kwa kuzichapa na Josh Warrington Oktoba 7 mjini Sheffield.

Wood, 34, alilipa kisasi kwa kumchapa Mauricio Lara kwa pointi na kutwaa ubingwa huo mara mbili katika pambano lake la mwisho lililofanyika Mei.

Bondia huyo mzaliwa wa Nottingham, alimuangusha chini Lara katika raundi ya pili na hakuonekana kuleta ushindani zaidi.

Warrington atapanda ulingoni akiwa na lengo la kutaka kutwaa mkanda huo wa Dunia kwa mara ya tatu.

Warrington, 32, ambaye ni mzaliwa wa Leeds, alipoteza mkanda wa IBF kwa kuchapwa na Luis Alberto Lopez kwa pointi katika pambano lililofanyika Desemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *