Wizara ya Kilimo kutoa mikopo ya bilioni 10 kwa Vijana na Wanawake.

Sarah Moses, Dodoma.

WIZARA ya Kilimo imepanga kutoa mikopo kwa vijana na wanawake kiasi cha Shilingi Bilioni 10 ikiwa ni ongezeko la bilioni 8 kutoka kiwango kilichoidhinishwa mwaka 2023/24 ili kuendeleza sekta ya kilimo kupitia Pembejeo, Uongezaji thamani pamoja na miundombinu ya Uwagiliaji

Hayo amesema Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa Mfumo wa Taifa  Pembejeo (AGITF) Fadhili Nyingi kwenye maonesho ya kilimo katika viwanja vya Bunge ambapo alisema mikopo hiyo itatolewa kwa mwaka 2024/2025.

Mikopo hiyo itatolewa kwa riba ya Asilimia 4.5 ili kuwezesha makundi ya vijana na wanawake wanaojihusisha na kilimo kuzalisha kwa tija ikiwa ni jitihada za serikali kuhakikisha kuwa mchango wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa Uchumi wa nchi kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

Amesema kuwa utoaji wa mikopo ulianza katika mwaka wa fedha uliopita ambapo mfumo wa Pembejeo ulikuwa umetengewa kiasi cha shilingi bil. 2.9 kwaajili  yakutoa mikopo na katika kipindi kilichopita wametoa mikopo zaidi ya 100 kwa vijana ambapo wameanza kutoa marejesho.

“Wengine wamesharudisha kabisa ambapo wameanza kuomba tena mikopo mikubwa zaidi kwahiyo jambo hili limebadili maisha hayo” amesema.

Wakati huo huo kwa upande wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Nchini TFRA Imeeleza namna upatikanaji wa ruzuku ya Mbolea kwa mwaka 2022/23 na 2023/24 umechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini kwa zaidi ya Tani milioni tatu.

Meneja Ununuzi wa Mbolea  kwa pamoja TFRA Elizabeth Bole amesema kuwa matumizi ya Mbolea yanachochea kuongeza uzalishaji na tija kwenye sekta ya kilimo .

“Mfano msimu wa 2021/2022takribani tani  mil.30 za mazao zilizaliswa lakini 2022/2023 uzalishaji uliongezeka Na kufikia takribani tani  mil.36 na tunatarajia kwa msimu huu kwa ongezeko hili la mbolea uzalishaji utaongezeka” amesema

Naye Afisa Kilimo Mkuu Wizara hiyo Justa katunzi amesema wamejaribu kufanya tathmini kidogo ya Wizara ya Kilimo ambapo  wamegundua kwa Mikoa na watu waliowapitia  wamesema wameridhika kwa huduma zinazotolewa  kwa asilimia 32 .

“Na hii ni kwakuwa tumeanza mwaka jana kwa kuwekeza katikabkuboresha huduma za ufanisi na za Kilimo ,tunaamini tunapokwenda katika miaka miwili hadi ni tatu hali yakufikia huduma kwa wananchi ” amesema Katunzi.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *